ASUBUHI (#11209)

Nimeamka katika himaya Yako, Ee Mungu wangu, na imembidi Yule ambaye anatafuta himaya hiyo kudumu ndani ya kimbilio la hifadhi Yako na Ngome ya Kinga Yako.  Angaza moyo wangu, Ee Bwana wangu, kwa utukufu wa Mapambazuko ya Ufunuo Wako kama ulivyoangaza mwili wangu kwa mwangaza wa asubuhi wa fadhili Yako.

-Bahá'u'lláh
-----------------------

ASUBUHI (#11210)

Nimeamka asubuhi hii kwa rehema Yako, Ee Mungu wangu, na nimeacha maskani yangu nikiwa na tumaini kamili Kwako, na nikijiweka katika uangalizi Wako.  Nishushie basi, kutoka mbingu ya rehema Yako, baraka kutoka ubavuni Mwako, na Uniwezeshe kurudi maskani mwangu katika usalama kama Ulivyoniwezesha kuondoka nikiwa chini ya ulinzi Wako na mawazo yangu yakiwa yamekaziwa kabisa juu Yako. 
 
   Hakuna  Mungu  mwingine  ila  Wewe,  Mmoja, Asiyelinganishwa, Ajuaye Yote, Mwenye hekima zote.

-Bahá'u'lláh
-----------------------

